Mhe. Hussein M. Bashe (Mb) Waziri wa Kilimo Aprili 17,2023 Jijini Dodoma amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu(TPHPA) na kuitaka bodi hiyo kuisimamia Mamlaka hiyo kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na kwa manufaa ya sekta ya Kilimo.
Mhe Bashe (Mb), ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya TPHPA kuhakikisha inajikita katika kuwezesha biashara ya mazao ya kilimo nje ya nchi, kuhakikisha inaimarisha kilimo anga hapa Nchini, pia kutumia teknolojia katika kukabiliana na visumbufu mimea na mazao.
Aidha, ameiagiza TPHPA kuwafutia leseni wafanyabiashara wote wa viatilifu ambao walifutiwa lesseni na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea kwa Kughushi katika biashara ya mbolea
Kwa upande mwingine ameitaka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kufanya usajili upya (Re-registration ) wa viuatilifu vyote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kudhibiti viuatilifu visivyo na ubora nchini.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)