• Contact us
  • FAQ
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)

The United Republic of Tanzania

Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)

Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
  • About us
    • Mission and Vision
    • Who we are
  • Services
    • Research and Consultancy
    • Pesticides Managment Control
      • Pesticides Registration Procedures
      • Procedures for carrying out Pesticides Business
      • Registered Pesticides in Tanzania
    • Technical Services
  • Administration
    • Board of Directors
    • Director General
      • Legal Services Unit
      • ICT and Statistics Unit
      • Internal Audit Unit
      • Pesticides Registration and Control Unit
      • Procurement Management Unit
      • Public Relations and Communication Unit
    • Organization Structure
    • Directorates
      • Directorate of Technical Services (DTS)
        • Pesticides Management and Environmental
          • Toxicology
        • National Herbarium of Tanzania Section
        • Post entry plant Quarantine Section
        • National Plant Genetic Resources Centre Section
      • Directorate of Corporate Services (DCS)
        • Finance and Accounts Section
        • Planning, Monitoring and Evaluation Section
        • Administration and Human Resources Management Section
      • Directorate of Research (DR)
        • Crop Protection
        • Diseases and Vector Control
  • Publications
    • 2019
  • Contact
  • Tender
  • Vacancy
  • Media Centre
    • Press Relases
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
  • Training
    • Vector Managment
    • Pests Managment
  • TPRI Scientist Profile

Mheshimiwa Anthony Mavunde Waziri wa Kilimo Azindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini.

Posted On: September 21st, 2022

SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani (FAO) na Umoja wa Ulaya (EU) imezindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini.

Akizungumza leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mradi huo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema mradi huo utasaidia katika kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia au kutoka hapa nchini yanakuwa na ubora unaokidhi viwango vya kimataifa.

Mavunde amesema kuwa mradi huo una lengo la kuhakikisha usalama wa Chakula na kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa usafi wa Mazao yanayoingia na kutoka nchini.

“Niwashukuru EU na FAO kwa kufadhili mradi huu muhimu ni imani yetu kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa na hivyo kuongeza upatikanaji wa masoko ya kimataifa na kuchochea uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja” amesema Mhe. Mavunde.

Amesema mradi huo umetokana na ukaguzi uliofanyika nchini mwaka 2017 katika mifumo maalumu ya udhibiti wa mimea na mazao yanayosafirishwa kwenda nchi za jumuiya ya Ulaya na ukaguzi huo kubaini mapungufu ya afya ya mimea.

Aidha Mavunde ametaja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na mapungufu hadi kupelekea kuanzishwa kwa mradi huo ni maarifa madogo kwa wakaguzi kuhusu matakwa ya usafi wa mazao hayo, kukosekana kwa mfumo kukusanya takwimu za visumbufu vya mimea, kukosekana kwa maabara zenye uwezo wa kufanya uchunguzi muhimu ili kuthibiti cheti cha usafi wa mimea. “kufuatia kubainika kwa mapungufu hayo na gharama za kufanya biashara ya mazao kuwa juu serikali ilichukua hatua kwa kuunganisha majukumu ya TPRI na ya afya ya mimea na viwatilifu TPHPA ambacho kimekuwa ni chombo kinachotambilika kimataifa” ameeleza Mavunde.

Hata hivyo ameeleza kuwa kuja kwa mradi huu utawezesha kufikia malengo ya kuhakikisha ukuaji wa sekta ya kilimo hapa nchini kwa asilimia 10 na mauzo ya mazao ya kilimo yanaongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 za sasa hadi kufikia Dola bilioni 5 ifikapo mwaka 2030. Amesema Wizara ya Kilimo itasimamia utaratibu na kuongeza utekelezaji wa mradi huo na kutaka kamati ya kusimamia mradi huo na kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kuwasimamia wataalamu ili kazi zilizopangwa kwenye mradi zitekelezeke kwa wakati.

Awali Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Obadia Nyagilo amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mika mitatu na nusu kwa kiasi cha Euro milioni 10.1 kwa ushirikiano ambapo Jumuiya ya umoja wa Ulaya itatoa Euro milioni 9.5, FAO itatoa Euro 350’000 na Tanzania itatoa EURO 250,000.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viwatilifu Tanzania TPHPA Dkt. Efraim Njau amesema sekta ya kilimo ni muhimu sana ambapo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa. Ametaja baadhi ya majukumu yanayofanywa na TPHPA ni kusimamia na kuratibu tasnia nzima ya viuatilifu, kudhibiti ubora, uagizaji, usambazaji na kuchagiza matumizi sahihi na usalama wa viuatilifu, kufanya uchambuzi wa athari ya visumbufu. Ameongeza kuwa “matokeo tarajiwa ya mradi huo ni kuziongezea uwezo maabara za mamlaka kujenga, kukarabati na kuweka vifaa katika maabara za Mamlaka, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa visumbufu na masalia ya viuatilifu katika mnyroro wa thamani ya uzalishaji wa mazao hususa ni yale mbogamboga na matunda” amesema Dkt. Njau.

Aidha amesema mradi utakuwa na kamati ambayo itaundwa na itawajibika kukutana na mara mbili kwa mwaka kupitia na kuhakikisha malengo ya mradi yanakwenda kama yalivyopangwa.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bi. Nyebenyi Tipo amesema mradi huo umelenga kuhakikisha usalama wa Chakula hasa kwa mazao yanayovuka mipaka kwa kuhakikisha yanakuwa na ubora na kuhakikisha usalama wa chakula na FAO watatoa ushirikiano kuhakikisha mradi huo unatekelezeka na unaleta tija kwa kukuza sekta ya kilimo na mazao ya hapa nchi kupata soko nje.

Announcements

  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU TANZAINIA KWA MWAKA 2022/2023 -March 10, 2023
  • More Announcements
  • Uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania -February 14, 2023
  • More Announcements
  • MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU MAKAO MAKUU YA TPHPA NGARAMTONI ARUSHA,TAREHE 07/11-18/11/2022 -October 07, 2022
  • More Announcements

Latest News

  • Mkutano wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Joseph Ndunguru na Vyombo vya Ha..

    March 10th, 2023
  • More News
  • Ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Joseph Ndunguru katika kituo cha A..

    March 10th, 2023
  • More News
  • Mamlaka yapokea Pikipiki kumi na tisa (19) aina ya Honda Maalumu kwa ajili ya sh..

    September 29th, 2022
  • More News
  • Mheshimiwa Anthony Mavunde Waziri wa Kilimo Azindua mradi wa kuimarisha huduma z..

    September 21st, 2022
  • More News

Contact Us

    Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)

    P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania

    Nairobi Rd, Ngaramtoni Area

    Fax : +255 272970468

    Telephone : +255 272970467 / 64

    Email : dg@tphpa.go.tz


Quick Links

  • Agricultural Trade Managment Information System (ATMIS)
  • Instagram
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Government e-Payment Gateway - SP Portal
  • Web Mail
  • List of registered pesticides to date
  • Pesticides Stock Managment System (Registered Pesticices, Whole sale, Retailers, Importers and Fumigators)
  • Tpri Library

Related Links

  • TARI Ukiriguru
  • Ministry of Agriculture
  • Sokoine University of Agriculture
  • Selian Agricultural Research Institute
  • Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH )
  • National Electoral Commision
  • Naliendele Agricultural Research Institute (NARI)

Recent Video

More Videos
  • Disclaimer
  • Privacy policy

Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)