Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea nchini.
Hayo yameelezwa leo Machi 01,2023 Katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru wakati akiongea na Vyombo vya Habari kuelezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo kwa mwaka 2022/2023.
Prof. Ndunguru amesema kuwa Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.
“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea,”amesema Prof.Ndunguru
Aidha Prof.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.
“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea,” amesema Prof.Ndunguru
Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na Mamlaka hiyo ,Prof.Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango.
Na kusema kuwa Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji
198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu.
''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 Mapato kiasi cha TZS Bilioni 3.06 Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu''Amesema Ndunguru.
Aidha amesema Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming”na kutumia Matokeo ya uchambuzi yatawezesha kutoa ushauri kulingana na eneo husika.
Majukumu ya mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu ni Kuwezesha biashara ya mimea na mazao ya mimea hapa nchini na kimataifa Pamoja na Kudhibiti uagizaji, usafirishaji, utengenezaji, usambazaji, uuzaji, matumizi ya viuatilifu na vifaa vya unyunyiziaji wa viuatilifu.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)