Mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu (TPHPA) wameratibu na kutoa mafunzo ya siku mbili juu ya afya ya mimea, uhifadhi wa viuatilifu pamoja na matumizi sahihi ya viuatilifu katika mazao ya horticulture.
Mafunzo hayo yamehusisha matumizi sahihi ya vifaa vya kupigia na umwagiliaji wa viuatilifu (bomba za kupigia dawa), mavazi ya kuvaa wakati wa kutumia viuatilifu na namna ya kusoma vibandiko (label) katika viuatilifu .
Mafunzo haya yamehusisha wakulima wa Mkoa wa Arusha kutoka kata mbalimbali zikiwemo kata za Nkoaranga, Imbaseni, Maji ya chai, Nkoanekoli, Nduruma, Ilikiding’a, Poli na Usa River.
Lengo la mafunzo haya ilikua ni kutoa elimu ya namna sahihi ya matumizi na uhifadhi wa viuatilifu ili kupunguza athari za kiafya kwa binadamu, wanyama na mimea zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu.
Hatua hii itasaidia pia kukidhi na kufikia viwango vya ubora na usalama wa chakula vinavyo hitajika na masoko ya ndani na nje huku ikizingatia utunzaji wa mazingira.
Mafunzo haya yameanzia Arusha na yataendelea Mikoa mingine Nchini.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)