Mtafiti wa TPRI Kitengo cha kuzuia visumbufu katika mimea, Ramadhan Kilewa alitoa semina ya uelewa juu ya kupambana na gugu karoti (Parthenium) ambalo limeonekana kuwa na madhara makubwa kwa binadamu, wanyama ,uoto wa asli, mimea na mazingira kwa ujumla. Semina hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa TPRI na imehudhuriwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na wadau kutoka NGOs na mashirika mbali mbali wanao husika na shughuli za mazingira. Ramadhani Kilewa alieleza kwa kina kuwa gugu karoti linato sumu ya Parthenin ambayo husababisha ugonjwa unaouitwa Parthenium allergic demartitis kwa binadamu.Pia alieleza madhara kwa wanyama ikiwemo manyonyo kunyonyoka, kupunguza ladha ya nyama,kupunguza uzalishaji maziwa na kusababisha kifo. Kwa uoto wa asili madhara ni kama kuzuia kuta mbegu na ukuaji wa mimea ya asili, kupunguza malisho ya wanyama, na kuleta athari virutubisho katika udongo. Kwenye mazao huzuia mbegu kuota, hupunguza ukuaji wa mazao, hupunguza mavuno ya mazao. Ramadhan Kilewa kutokana na tafiti alizofanya alienda mbali zaidi na kuelezea hatua madhubuti za kuteketeza gugu karoti kwenye uso wa dunia ikiwemo kuzuia kuenea katika maeneo ambayo halija samba, kung’oa gugu karoti kabla ya kumea na kutoa maua na mbegu kisha choma moto, kutumia viuagugu (herbicides ). Pia alisisitiza kuchuchua tahadhari kama vile kuvaa masks na gloves ili kuzuia vumbi ya maua kutoka kwenye gugu karoti isikuingie na pia alisema ni vyema ukihisi mwasho au hali ya kuchomachoma kwenye ngozi unapaswa kunawa haraka na maji ya baridi sehemu husika na sio kujikuna.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)