Washiriki wa Mafunzo ya Taaluma Maalumu ya Viuatilifu yaliyofanyika Mjini Mwanza, mafunzo yaliyoendendeshwa na Wataalamu kutoka Taasisi ya udhibiti wa Viuatilifu " Tropical Pesticides Research Institute (TPRI)" Arusha wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo shamba la MAHINDI wakijifunza utambuzi wa uwepo wa wadudu/visumbufu vamizi kama vile viwavijeshi na namna sahihi ya kutumia viatilifu ili kuwaangamiza na hatimae kufanya kilimo chenye tija. Pia Mratibu wa Mafunzo Ndugu Jumanne Rajabu kutoka TPRI aliwahasa washiriki kufanya kilimo kwa mfumo wa "Shamba ofisi", hapa alimaanisha kuwa wakulima wanapaswa kuwapo shambani muda mwingi ili waweze kufuatilia kwa karibu kilimo wanachofanya na kuwanya utambuzi wa uwepo wa viashiria vya wadudu/visumbufu na kudhibiti katika hatua za awali kwa kutumia viuatilifu sahihi na kwa wakati, hii itamwepusha kutumia nguvu nyingi na gharama kubwa kudhibiti wadudu/visumbufu ikiwa wameshasababisha madhara.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)