Washiriki wa Mafunzo ya Taaluma Maalumu ya Viuatilifu wakiwa wanajifunza Mfumo mpya wa Tehama unaoitwa “Agricultural Trade Management Information System (ATMIS)”. Mfumo huu unamsaidia mfanyabiashara ya Viuatilifu Kujisajili, Kutuma maombi ya Vibali ya biashara za Viuatilifu, Kulipia kwa kutumia Namba ya kumbukumbu (Control Number) na kupata Vibali vya Kielektroniki kwenye mtandao pasipo wafanyabiashara kufika TPRI. Mfumo huu una faida nyingi ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa vibali, kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara, kuongeza uwajibikaji, kurahisisha ufuatiliaji,kudhibiti udanganyifu, kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi zinazotozwa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu kwa mujibu wa sharia na kanuni ya viuatilifu (Plant Protection Act 1997) na Kanuni zake (Regulation 1999) na pia kuwezesha uhifadhi na upatikanaji wa taarifa za wadau wote wa Viuatilifu nchini Tanzania.
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)