Washiriki wa Mafunzo ya Taaluma Maalumu ya Viuatilifu yaliyofanyika Mjini Mwanza, mafunzo yaliyoendendeshwa na Wataalamu kutoka Taasisi ya udhibiti wa Viuatilifu "Tropical Pesticides Research Institute (TPRI)" Arusha wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo kwenye shamba la PAMBA wakijifunza utambuzi wa wadudu / visumbufu vamizi na namna sahihi ya unyunyuziaji wa viuatilifu ili kuepusha uchafuzi wa mazingira. Pia washiriki walijifunza namna ya kutumia nozeli za kuangamiza magugu na nozel za kuangamiza wadudu / visumbufu kwenye shamba la PAMBA na pia walipata nafasi ya kujionea madhara yanayotokana na kuzidisha kiwango cha viuatilifu kwenye zao la pamba, Washiriki hao walifurahihwa na utaalamu huo na kuahidi kutumia taaluma hiyo kwenye zao la pamba kwa kuwa msimu wa pamba utaanza hivi karibuni na ndio zao kuu la biashara kwenye ukanda wa ziwa victoria ambapo linaiongeza Serikali pato la Taifa
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)