Tokisolojia ni elimu ya sayansi ya sumu. Sumu ni chochote kile kiwezacho kuleta madhara ya kiafya kinapoliwa kupitia mdomoni, kinapoingia kupitia ngozi ya mwili na kinapovutwa kwa njia ya hewa na mara nyingine kwa kupitia mfuko wa mimba (transfer across placenta)
90% ya sumu zote huingia mwilini kwa njia ya ngozi, na hii ndiyo njia ya hatari zaidi kuliko zote. Sumu ikiisha kuingia mwilini husambaa kupitia mfumo wa damu na kusababisha madhara katika maeneo maalum (target cells) hasa mishipa ya fahamu (Nerves) na kusababisha “Neurological disease” pale kimengenyo cha Kolinesterasi “Cholinesterase” kinapozuiliwa kufanya kazi na utendaji wake kupunguzwa “depression” hii husababisha dalili za sumu kuonekana mwilini mfano kichwa kuumwa, kutapika, kichefuchefu,misuli kugangamaa, tumbo kuumwa na pia kushindwa kupumua vizuri.
Ni vigumu mno kukwepa sumu zisiingie mwilini mwetu, kwani kwa kufanya hivyo, tutalazimika tusivute hewa wala tusinywe maji na pia tusile chakula na kuvuta hewa. Hii ina maana kila mtu anaishi na sumu ndani ya mwili lakini viwango vyake havipaswi kuwa juu ya viwango salama (Threshold level) ili kuruhusu mwili kuhimili (NOEL). Katika kiwango hiki (Non-observable Effect level) hakuna dalili zozote za sumu zinazoonekana na sumu huliwa kama chakula mfano, Hifadhi ya vinywaji (Preservative) kemikali hutumika bila madhara kwa wanywji. Hii hutokana na jibu la NOEL kugawanywa kwa kiwango kilicho salama cha 100 au 1000 (safety factor of 100 or 1000) ili kupata ADI (Aceptable daily intake).
Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)
P.O. Box 3024 , Arusha - Tanzania
Nairobi Rd, Ngaramtoni Area
Fax : +255 272970468
Telephone : +255 272970467 / 64
Email : dg@tphpa.go.tz
Copyright ©2016 Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA). All rights reserved.
Designed and Developed by: e-Government Authority (eGA). Content maintained by: Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA)